(Kinyarwanda) KUSHUTUMU VITENDO VYA KIGAIDI VYA UTAWALA WA KIGALI NA KUDAI HAKI KWA WAHANGA WA MAUWAJI YA KIMBARI NA UHALIFU MWINGINE MKUBWA ULIOFANYWA NA KUNDI LA RPF (RWANDAN PATRIOTIC FRONT) KATIKA ENEO LA MAZIWA MAKUU

GVRRswa
 • Views 848
 • Rating 12345

Sorry, this entry is only available in Kinyarwanda. For the sake of viewer convenience, the content is shown below in the alternative language. You may click the link to switch the active language.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA (Global Voice of Rwandan Refugees, GVRR), Shirika ambalo lengo lake ni kukemea vitendo vya unyama ulio fanywa zidi ya wakimbizi wa Rwanda na kusikilizisha sauti zao, kufatilia kwa hamu kubwa hali ambayo imeenea katika eneo la maziwa makuu ya Afrika kuanzia tarehe ya 1 octoba 1990, nakulaani vikali vitisho na vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na serikali ya Kigali (i.e. RPF/APR) zidi ya wateteyaji wa haki za binadamu na watu wengine wanaofanya kampeni ya kuimarisha ukweli na kudai haki kwa wahanga wote wa uhalifu uliofanywa katika eneo hilo tangu tarehe ya 1 octoba 1990 hadi leo.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA inalaani kwa nguvu zote vitisho vya maajenti wa mamlaka ya Kigali na haswa yale yaliyotolewa na jenerali JAMES KABAREBE, mshauri maalumu wa Rais PAUL KAGAME, alilenga kumtisha mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Daktari DENIS MUKWEGE kwa ajili aachane na ombi analo endelesha akidai umoja wa mataifa (UN) ishugulikie na kuchukuwa hatuwa juu ya hitimisho la ripoti ya mapping iliyochapishwa mnamo oktoba 2010, ambayo inaitimu ualifu uliofanywa na RPF zidi ya wakongomani na wakimbizi wahutu kama uhalifu zidi ya binadamu, uhalifu wa kivita, hata mauwaji ya kimbari.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA inachukuwa fursa hii kulaani sera ya utawala wa Rwanda ya vitisho unyanyasaji, kifungo na kuondolewa kwa mtu yeyote anaetaka kutoa mwangaza juu ya dhulma zilizofanywa na RPF/APR. Sera hii inatetewa vikali na kutekelezwa kupita uwakilishi za vikosi vya vifo (death squads) vinavyo husika na mauwaji ya wapinzani wa utawala wa kigali. Mfano wa kushangaza zaidi ni ule wa ubalozi wa Rwanda, nchini Afrika kusini munamo machi 2014, kwa kuhusika kwao katika mauti ya hayati kanali PATRICK KAREGEYA. Mabalozi waliojitambulisha katika kazi hii chafu ni Bwana VINCENT KAREGA, balozi wa sasa wa Rwanda nchini Democratic Republic of the Congo (DRC), Bwana JEAN-CLAUDE NIKOBISANZWE, balozi wa sasa nchini Msumbiji (Mozambique) na Bwana OLIVIER NDUHUNGIREHE, balozi wa zamani wa Rwanda nchini ubelijiji (Belgium). Walikuwa wa kwanza kuunga mkono maneno ya jenerali JAMES KABAREBE, kumtisha mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Daktari DENIS MUKWEGE. Ikumbushwe kwamba kesi ya Daktari DENIS MUKWEGE siyo ya kwanza kwa sababu, hata viongozi wengine wamekuwa waasiriwa wa sera hi ya mauwaji, tunaweza kutaja hasa :

 • Askofu mkuu MUNZHIIRWA MWENE NGABO, aliuwawa tarehe ya 29 oktoba 1996 huko Bukavu, na komando wa jeshi la Rwanda ambae alikuwa akishutumu vikali ukandamizi wa utawala wa Kigali na dhulma za harakati ya AFDL.
 • Askofu mkuu MUNZHIIRWA MWENE NGABO, aliuwawa tarehe ya 29 oktoba 1996 huko Bukavu, na komando wa jeshi la Rwanda ambae alikuwa akishutumu vikali ukandamizi wa utawala wa Kigali na dhulma za harakati ya AFDL.
 • Kasisi mchungaji CHRISTOPHER MTIKILA, mtanzania, aliuwawa mnamo 2015 kwa sababu ya ufunuo wake juu ya vitendo vya uhalifu vya kali kwa kuzingatia kuundwa kwa himaya ya HIMA-TUTSI katika eneo la afrika na mashariki.
 • Mtetezi CHEBEYA BAHIZIRE, aliuwawa mnamo tarehe 2 juni 2010 huko Kinshasa.
 • Daktari DENIS MUKWEGE alinusurika chupuchupu katika jaribio la kifo mnamo oktoba 2012. Wakati huo mlinzi wake wa nyumba yake, aliuwawa kwa kupigwa risasi.
 • Watu wengine ambao wamekuwa wakitishwa wazi ni Bwana JAKAYA MRISHO KIKWETE, rais mustaafu wa Tanzania, alitishwa wazi kuuwawa na rais KAGAME ; Bwana CHARLES ONANA, mwandishi wa habari, Bibi JUDI REVER, mwandishi wa habari ; marehemu PIERRE PEAN, mwandishi wahabari ; Bibi CARLA DEL PONTE mwendesha mashtaki wazamani wa ICTR, Bibi MASAKO YONEKAWA, ANJAN SUNDARAM, mwandishi wahabari ; Bwana FERNANDO ANDREU MERELLES, jaji wa Uhispaniya ; Bwana JEAN- LOUIS BRUGUIERE jaji wa Ufaransa ; Mchungaji Pastor PASCAL MUKUNA ; Mchungaji Pasta KUTINO FERNANDO,…

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA inaipongeza serekali ya DRC kwa uamuzi wake wakufungua uchunguzi na kuweka hatua za kuhakikisha usalama wa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ya 2018 Daktari Denis Mukwege.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA inashutimu tabia isiyofaa ya jamii ya kimataifa kuzika kwa utaratibu ripoti zote zilizo wekwa na Umoja Wa Mataifa (UN) ambazo zinashirikiana wazi mambo ya RPF, katika mauaji hayo. Kati ya ripoti muhimu ambazo zimebaki zimeziniwa, tunaweza kutaja :

 1. Ripoti ya GERSONY ya 1994, iliolenga mauaji (yalio stahiki kuitwa kama muaji ya kimbari) ya wahutu nchini Rwanda mnamo 1994,
 2. Ripoti ya ROBERTO GARRETON ya 1998, ilionyesha kuuawawa na kutoka kwa mamia ya ma elfu ya wakimbizi wa kihutu (warundi na wanyamurwanda) timu hii ya Umoja wa Mataifa (UN) ili chunguza karibu maeneo arubaini (40) inchini DRC na kuripoti juu ya maiti zaidi ya laki mbili (200 000) za wakimbizi wa Rwanda.
 3. Ripoti UN Mapping, ripoti hii ina uhalifu wa kimvumo na wakukusudie unaufanywa na RPF dhidi ya wa kongomani na wakimbizi wahutu (watoto wanawake wazee na wa gonjwa) ya uhalifu dhidi ya ubinadamu uhalifu wa kivita hata mauaji ya kimbiri.
 4. Kukataa kufanya uchunguzi mzito kwa jamii ya kimataifa, kutoa mwangaza juu ya wahusika halisi wa mauwaji mabaya ya marais JUVENAL HABYARIMANA wa Rwanda, CYPRIEN NTARYAMIRA wa Burundi, aliyotokea mnamo tarehe 6 April 1994. Tamko la «sio mahali » la mahakama ya Ufaransa ni dhihaka kwa wanafamilia wa waliopotea.
 5. Ukosefu wa uchunguzi zidi ya mauaji yaliyofanywa mnamo 1995 katika KAMBI ya KIBEHO nchini Rwanda ikiwepo chini ya ulinzi wa walinda amani wa Umoja Wa Mataifa (UN).
 6. Makusudi ya jamii ya kimataifa kufunika ukweli juu ya ualifu wa RPF ni ukeukaji mkubwa zidi ya utakatifu wa maisha ya wa asiriwa, ambayo inaashiriya mshikamano wa nguvu fulani katika matokeo mabaya ambayo yanaendelea kuliza watu wetu na kuendelea kuhoofisha utulivu katika inchi zetu.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA inahisi kuwa mashtaka ya kisheria ya wale waliohusika na vitendo vibaya ndio njia bora ya kutokomeza utamaduni wa kutokujali na kutuma ishara kali kwa wale wote ambao wana nia moja ya kuwaibia watu haki yao takatifu kwa maisha. Sheria kwa usawa ndio wokovu pekee kwa inchi yoyote inatamani utulivu na mshikamano wa kijamii kwa sababu hukumu ambazo zitatolewa bila shaka zitachangia kulipa uharibifu uliosababishwa kwa muhanga wa vitendo hivi vya vurugu.

Kwa kuzingatia kwamba wakimbizi wa Rwanda wana fikia maelfu, pamoja na kaka na dada zao wa Congo kati ya wahanga wa mauaji yaliofanyika na askari wa jeshi la RPF nchini DRC.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA ingependa kuungana sauti yake na wale wote wanaodai haki kwa wahanga wote wa vitendo hivi vya kinyama vya RPF. Katika swala hili GVRR inaunga mkono ombi la Daktari DENIS MUKWEGE kuwaona wale wote ambao wametajwa katika ripoti ya Mapping kujibu matendo yao mbele ya mahakama huru.

Hakika kwamba mshikamano kati ya watu ni ufunguwo na silaha kali zaidi ya maghaidi wanayo endesha ukeukaji wahaki za binadamu, vitendo vya kighaidi, mauwaji zidi ya raia. SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA inatowa shukran kubwa, natayari kuchangiya msaada wowote huyo kwa wale wote wanaofanya juhudi bila kuchoka kwa kuhakikisha kwamba ripoti zilizosimamishwa zishughulikiwe kisheria na wahusika waliyo sababisha vifo na uhalifu katika eneo la maziwa makuu wanafikishwa maakamani. Baadhi yahawo wateteaji ya haki za binaadamu tunawapongeza wakina : jumuiya ya Congo ya LUCHA ; FILIMBI ; MWAMKOO WA KIZALENDO (Eveil patriotique) ; ASASI ZA KIRAIYA KUTOKA KIVU KUSINI (Société civile Sud Kivu) ; ASASI ZAKIRAIYA KUTOKA KIVU KSAKAZINI (Société Civile du Nord Kivu) ; CENCO ; UMOJA WAWATU WAKIBANTU (UPB) ; Mhe. MARTIN FAYULU ; Askofu mukuu wa Bunia ; DIEUDONNE ULINGI ; Askofu PASCAL MUKUNA ; Mwanasheria JEAN CLAUDE KATENDE wa chama cha ASADHO, Bwana CHARLES ONANA ; Bibi JUDI REVER ; Bibi MASAKO YONEKAWA ; mshindi wa tuzo ya NOBEL Bwana ADOLFO PEREZ ESQUIVEL na watetezi wengine wahaki za binadamu na vilevile makasisi ambao hawaachi kutowa wito wahaki.

SAUTI YA WAKIMBIZI WA RWANDA ya zinduwa ombi la dharura kwa jamii ya kimataifa kukomesha kabisa upotovu wa utawala katika eneo la maziwa makuu tangu oktoba 1990 kwakuvunja ulinzi uliopewa utawala wenye kiburi na katili wa Kigali na kutekeleza itimisho ya ripoti zilizo tajwa hapo juu ili wahusika wote watambuliwe, washtakiwe na wawajibishwe kwa uhalifu wao.

SAUTI YA WA KIMBIZI WA RWANDA inawaalika wanaume na wanawake wote wanaopenda amani na haki ulimwenguni kote, kufwata nyayo za mushindi wa tuzo ya amani ya Nobel Daktari DENIS MUKWEGE katika juhudi zake za kuvunja muzunguko wavurugu kupitia haki sawa.

PAMOJA TUTASHINDA ḷ

IMEFANYWA CAPE TOWN, 3 SEPTEMBA 2020

JMV Nyilimbilima

Mwenyekiti wa GVRR

Print Friendly, PDF & Email
Share on FacebookTweet about this on TwitterEmail this to someone

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *